DEU_Kiswahili_1068.pdf

(261 KB) Pobierz
KUMBUKUMBU LA TORATI
Utangulizi
Kumbukumbu la Torati limetokana na neno la Kiyunani ‘’ Deuteronomion’’ ambalo maana yake ni ‘‘ kutolewa kwa amri
mara ya pili.‘’ Kitabu hiki kilipewa jina hili na watafsiri wa (Septuagint ), yaani, Agano la Kale kwa Kiyunani.Katika hotuba
zilizonakiliwa katika Kumbukumbu la Torati, Mose anafanya ufupisho wa dini ya Wairaeli kuwa agano lililotolewa kwa baba
zao wakuu kuwa ndilo msingi wa uhusiano ulioanzishwa na Mungu baina Yake na Waisraeli, wala si sheria, ambalo sasa
linadhihirishwa kwa Waisraeli kwa kuokolewa kutoka Misri na kutunzwa kwa muda wote wa kutangatanga huko jangwani.
Baada ya miaka arobaini, Waisraeli walikuwa wamekaribia kuingia katika Nchi ya Ahadi. Lakini kabla ya kufanya hivyo,
Mose alitaka kuwakumbusha historia yao, yaani, yale yote ambayo Mungu alikuwa amewatendea, pamoja na amri zile zote
walizopaswa kuendelea kutii kama taifa teule la Mungu.
Kusudi kubwa la Mose lilikuwa wao Waisraeli waitikie upendo wa Mungu kwa moyo wote.Hii ndiyo njia pekee ambayo
wangeweza kuendelea kufurahia upendeleo wa Mungu na baraka Zake.Upendo wa halisi kwa Muingu ungekuwa ushahidi
katika kicho na heshima kwa Mungu na kujitoa kwao Kwake.Hivyo kwa asili, wangetii maagizo ya kimungu yanayohusu
kuishi maisha matakatifu.
Mazungumzo ya kwanza ya Mose yalikuwa kuwakumbusha watu wema wa Mungu kwa kipindi chote cha safari ili
kuwapa nchi ya Kanaani. Mazungumzo ya pili yalikuwa ni muhtasari wa sheria za Mungu zikiwepo Amri kumi. Mose
aliwaambia watu ‘‘Mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa nguvu zako zote, ’’
(6 :5) ili waweze kuendelea kuzifurahia baraka za Mungu. Pia Mose alitilia mkazo ukweli kwamba ili waweze kuwa na
uhusiano mzuri na Mungu, ilikuwa ni lazima watu wawafundishe watoto wao kumpenda Mungu na kuzitii amri zake.
Kutokana na hilo haki na uadilifu ungepenya katika maisha yao ya kila siku, kadiri ambavyo upendo wao ungeelekezwa
kwa ndugu wa kiume na wa kike.
Ili kudumisha uhusiano huu muhimu wa upendo kati ya Waisraeli na Mungu, wazazi waliagizwa kuwafundisha watoto
wao (4 :9-10 ; 6 :7) kumcha Mungu kwa mafundisho na kwa kielelezo. Kwa njia ya kuadhimisha zile sikukuu za mwaka,
yaani, Pasaka, Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu,Sikukuu ya Majuma, Sikukuu ya Vibanda, Pentekoste, pamoja na yale
makusanyiko mengine, Waisraeli walivikumbusha vizazi vingine vilivyofuata juu ya upendo wa Mungu ulioonyeshwa
kwenye ukombozi wao toka Misri na kuendelea kwao kutunzwa Naye kwa kuwapa mazao.
Kumbukumbu la Torati linaishia likiwakumbusha Waisraeli juu ya agano ambalo Mungu alifanya nao (Kumbukumbu la
Torati 29), kuteuliwa kwa Yoshua kuwa kiongozi mpya (Kumbukumbu la Torati 31) na kifo cha Mose ( Kumbukumbu la
Torati 34).
Wazo Kuu
Kuwakumbusha Waisaeli juu ya agano la Mungu na baba zao, kuwapa mwongozo jinsi ya kudumisha hilo agano kwa
kumpenda Mungu kwa moyo wote na kuwapenda wengine.Upendo na utii ndio mkazo mkuu katika kitabu hiki.
Mwandishi
Inakubalika kwamba Mose ndiye aliyeandika kitabu hiki isipokuwa hii sura inayoelezea juu ya kifo chake.
Tarehe
Kiliandikwa kama 1645 K.K.
Mahali
Kaitka nchi tambarare ya Moabu, Mashariki mwa mto Yordani, karibu na Yeriko, wakiwa wanaikabili nchi ya Kanaani, kabla
tu ya kuvuka kuingia (1 :5 ; 34 :1-12) .
Wahusika Wakuu
Mose, Yoshua na Waisraeli
Mgawanyo
Mazungumzo ya kwanza ya Mose. (1:1-4:43)
Mazungumzo ya pili ya Mose. (4:44-11:32)
Sheria za maisha ya kila siku. (12:1-26 :29)
Matokeo ya kutii na kutokutii. (27:1-28:68)
Kufanya upya agano. (29:1-30:20)
Baraka za Mose kwa Israeli na kifo chake. (31:1-34:12)
KUMBUKUMBU LA TORATI
Amri Ya Kuondoka Mlima Horebu
Haya ni maneno Mose aliyoyasema kwa
Israeli yote jangwani mashariki ya
Yordani, ambayo iko katika Araba inayokabiliana
na Sufu kati ya Parani, Tofeli, Labani, Hazerothi
na Dizahabu . 2 (Ni mwendo wa siku kumi na
moja kutoka Horebu kwa njia ya Mlima Seiri
mpaka Kadesh Barnea.
3 Katika mwaka wa arobaini, siku ya kwanza
ya mwezi wa kumi na moja, Mose aliwatangazia
Waisraeli yale yote BWANA aliyomwamuru
kuwahusu. 4 Hii ilikuwa ni baada ya kumshinda
Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala
Heshboni na huko Edrei alikuwa amemshinda
Ogu mfalme wa Bashani, ambaye alitawala
huko Ashtarothi. 5 Huko Mashariki ya Yordani
katika nchi ya Moabu,Mose alianza kuielezea
sheria hii, akisema:
maafisa wa makabila. 16 Nami wakati ule
nikawaagiza waamuzi wenu: “Sikilizeni magomvi
kati ya ndugu zenu na mwamue kwa haki, hata
kama shauri ni kati ya ndugu wa Kiisraeli au kati
ya mmoja wa ndugu wa Kiisraeli na mgeni.
17 Msionyeshe upendeleo katika maamuzi,
wasikilizeni wote sawasawa, wadogo na
wakubwa. Msimwogope mtu ye yote kwa kuwa
hukumu ni ya Mungu, mniletee mimi shauri lo
lote lililo gumu sana kwenu, nami nitalisikiliza.
18 Nami wakati ule niliwaambia kila kitu ambacho
mngefanya.
Wapelelezi Wanatumw a
19 Kisha, kama BWANA Mungu wetu
alivyotuamuru, tuliondoka kutoka Horebu na
kwenda kuelekea nchi ya vilima ya Waamori
kupitia jangwa lile kubwa lote la kutisha, lile
mliloliona,nasi tukafika Kadeshi-Barnea. 20 Kisha
niliwaambia, “Mmefika katika nchi ya vilima ya
Waamori, ambayo BWANA Mungu wetu
anatupa. 21 Tazama, BWANA Mungu wenu
amewapa nchi. Pandeni mkaimiliki kama
BWANA, Mungu wa baba zenu, alivyowaambia.
Msiogope wala msikate tamaa.’’
22 Ndipo ninyi nyote mkanijia na kusema,
“Tupeleke watu watutangulie kuipeleleza nchi
kwa ajili yetu na kutuletea taarifa kuhusu njia
tutakayopita na miji tutakayoiendea.’’
23 Wazo hilo lilionekana zuri kwangu, kwa
hiyo niliwachagua watu wenu kumi na wawili,
mwanaume mmoja kutoka kila kabila.
24 Waliondoka na kukwea katika nchi ya vilima,
wakafika katika Bonde la Eshkoli na kuipeleleza.
25 Wakachukua baadhi ya matunda ya nchi,
wakatuletea na kutuarifu. “Ni nchi nzuri ambayo
BWANA Mungu wetu anatupa.’’
1
6 BWANA Mungu wetu alisema nasi huko
Horebu, ‘Mmekaa vya kutosha katika mlima huu.
7 Vunjeni kambi msonge mbele kuelekea katika
nchi ya mlima wa Waamori, nendeni kwa watu
wote ambao ni majirani wa Araba, katika milima,
upande wa magharibi chini ya vilima, katika
Negebu na kandokando ya pwani mpaka nchi ya
Wakanaani hadi Lebanoni, na kufika mto
mkubwa Eufrati. 8 Tazama, nimewapa ninyi nchi
hii. Ingieni mkaimiliki nchi ambayo BWANA
aliapa kuwa angaliwapa baba zenu, Abrahamu,
Isaki na Yakobo pamoja na vizazi vyao baada
yao.’ ”
Uteuzi Wa Viongozi
9 Wakati ule niliwaambia, “Ninyi mmekuwa
mzigo mzito sana kwangu kuwachukua peke
yangu. 10 BWANA Mungu wenu ameongeza
hesabu yenu kwamba leo ninyi ni wengi kama
nyota za angani. 11 Naye BWANA Mungu wa
baba zenu, na awaongeze mara elfu na
kuwabariki kama alivyoahidi! 12 Lakini mimi
nitawezaje kubeba matatizo yenu na mizigo
yenu na magomvi yenu peke yangu?.
13 Chagueni baadhi ya watu wenye hekima,
wenye ufahamu na wanaoheshimika kutoka
katika kila kabila lenu, nami nitawaweka juu
yenu.”
14 Mlinijibu, “Shauri ulilolitoa ni zuri.’’
15 Kwa hiyo niliwachukua wanaume viongozi
wa makabila yenu, wenye hekima na
wanaoheshimika, nami nikawateua wawe na
mamlaka juu yenu kama majemadari wa maelfu,
wa mamia, wa hamsini na wa makumi na kama
Uasi Dhidi Ya BWANA
26 Lakini hamkuwa tayari kukwea, mkaasi
dhidi ya amri ya BWANA Mungu wenu.
27 Mkanun’gunika ndani ya mahema yenu na
kusema, “BWANA anatuchukia, kwa hiyo
alitutoa Misri ili kututia mikononi mwa Waamori
kutuangamiza. 28 Twende wapi? Ndugu zetu
wametufanya kufa moyo. Wanasema, ‘Watu wa
huko wana nguvu zaidi na ni warefu kuliko sisi
tulivyo, miji ni mikubwa, yenye kuta zilizofika juu
angani. Zaidi ya hayo tumewaona Waanaki
huko.’ ’’
29 Ndipo nikawaambia, “Msihofu, wala
msiwaogope.
30
BWANA
Mungu
wenu
anayewatangulia, atawapigania, kama
2
952103022.004.png
 
KUMBUKUMBU LA TORATI
alivyofanya kwa ajili yenu huko Misri, mbele ya
macho yenu hasa, 31 pia huko jangwani. Huko
mliona jinsi BWANA Mungu wenu
alivyowachukua, kama baba amchukuavyo
mwanawe, katika njia yote mliyoiendea mpaka
mkafika mahali hapa.”
32 Pamoja na hili, hamkumtegemea BWANA
Mungu wenu, 33 ambaye aliwatangulia katika
safari yenu, kwa moto usiku na kwa wingu
mchana, kuwatafutia mahali penu pa kupiga
kambi na kuwaonyesha njia mtakayoiendea.
34 Wakati BWANA aliposikia lile mlilosema,
alikasirika akaapa, akasema: 35 “Hakuna mtu wa
kizazi hiki kiovu atakayeona nchi nzuri niliyoapa
kuwapa baba zenu, 36 isipokuwa Kalebu mwana
wa Yefune. Yeye ataiona, nami nitampa yeye na
wazao wake nchi aliyoikanyaga kwa miguu, kwa
sababu alimfuata BWANA kwa moyo wote.”
37 Kwa sababu yenu BWANA pia
alinikasirikia mimi akasema, “Hutaingia hiyo nchi
pia. 38 Lakini msaidizi wako, Yoshua mwana wa
Nuni, ataiingia. Mtie moyo, kwa sababu
atawaongoza Waisraeli kuirithi hiyo nchi . 39 Wale
watoto ambao mliwasema wangelichukuliwa
mateka, yaani watoto wenu ambao bado
hawajui jema na baya wataingia katika nchi.
Nitawapa hiyo nchi nao wataimiliki. 40 Bali ninyi,
geukeni, mwondoke kuelekea jangwani kwa
kufuata njia ya Bahari ya Shamu.’’
kuzunguka vilima katika nchi ya Seiri.
2 Kisha BWANA akaniambia, 3 ‘‘Umetembea
kuzunguka hii nchi ya vilima kwa muda wa
kutosha, sasa geukia kaskazini. 4 Wape watu
maagizo haya: ‘Mko karibu kupita katikati ya
nchi ya ndugu zako ambao ni wazao wa Esau,
ambao wanaishi Seiri. Watawaogopa, lakini
mwe waangalifu. 5 Msiwachokoze kwa vita kwa
maana sitawapa ninyi sehemu yo yote ya nchi
yao, hata sehemu ya kutosha kuweka wayo
wenu juu yake. Nimempa Esau nchi ya vilima ya
Seiri kama yake mwenyewe. 6 Mtawalipa fedha
kwa
chakula
mtakachokula
na
maji
mtakayokunywa.’ ’’
7 BWANA Mungu wenu amewabariki kwa
kazi yote ya mikono yenu. Amewalinda katika
safari yenu katikati ya jangwa hili kubwa. Kwa
miaka hii arobaini BWANA Mungu wenu
amekuwa pamoja nanyi na hamkupungukiwa na
kitu cho chote.
8 Basi tulipita kwa ndugu zetu wazao wa
Esau ambao wanaishi Seiri. Tuligeuka kutoka
njia ya Araba ambayo inatokea Elathi na Esion-
geberi, tukasafiri kufuata njia ya jangwa la
Moabu.
9 Kisha BWANA akaniambia, “Usiwasumbue
Wamoabi kwa vita, kwa kuwa sitawapa sehemu
yo yote ya nchi yao. Nimetoa nchi ya Ari kwa
wazao wa Loti kama milki yao.’’
41 Ndipo mkanijibu, “Tumemtenda BWANA
dhambi. Tutakwenda kupigana, kama BWANA
Mungu wetu alivyotuamuru.” Hivyo kila mmoja
wenu akachukua silaha zake, huku mkifikiri
kuwa ni rahisi kukwea katika nchi ya vilima.
42 Lakini BWANA aliniambia, “Waambie,
‘msipande kupigana, kwa sababu sitakuwa
pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu.’ ’’
43 Hivyo niliwaambia, lakini hamkutaka
kusikia. Mliasi dhidi ya amri ya BWANA na
katika kiburi chenu mlienda katika nchi ya vilima.
44 Waamori ambao waliishi katika vilima hivyo
waliinuka dhidi yenu, wakawafukuza kama kundi
la nyuki wakiwapiga njia yote ya Seiri mpaka
Horma. 45 Mlirudi na kulia mbele za BWANA,
lakini Mungu hakusikiliza kilio chenu, wala
hakuwajali. 46 Hivyo mlikaa Kadeshi kwa siku
nyingi, kwa muda wote mlikaa huko.
Kutangatanga Jangwani
Kisha tukageuka nyuma na kusafiri
kuelekea jangwani kwa njia inayoelekea
bahari ya Shamu, kama BWANA
alivyonielekeza. Kwa muda mrefu tulitembea
10 (Waemi walikuwa wakiishi huko hapo
zamani, watu wenye nguvu, wengi na warefu
kama Waanaki. 11 Kama walivyokuwa Waanaki,
hao pia walikuwa kama Warefai, lakini
Wamoabu waliwaita Waemi. 12 Wahori waliishi
Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafukuza.
Wakawaangamiza Wahori na kukaa mahali pao,
kama Waisraeli walivyofanya katika nchi
ambayo BWANA aliwapa kama milki yao.)
13 BWANA akasema, “Sasa ondokeni mvuke
Bonde la Zeredi.” Hivyo tukavuka bonde.
14 Miaka thelathini na minane ilipita tangu
wakati tulipoondoka Kadesh-Barnea mpaka
tulipovuka Bonde la Zeredi. Kwa wakati huo kile
kizazi chote cha wanaume kuanzia wale
wawezao kwenda vitani kilikuwa kimekufa, kama
BWANA alivyokuwa amewaapia. 15 Mkono wa
BWANA uliwakabili hadi alipowaangamiza wote
huko kambini.
16 Ikawa baada ya mtu wa mwisho kuanzia
wale wawezao kwenda vitani, kufa, 17 BWANA
akaniambia, 18 “Leo utapita katika nchi ya Moabu
huko Ari. 19 Utakapokuja kwa Waamori,
msiwasumbue wala kuwachokoza kwa vita, kwa
2
3
952103022.005.png
 
KUMBUKUMBU LA TORATI
kuwa sitawapa ardhi yo yote iliyo ya Waamori
kuwa milki yenu. Nimeitoa kama milki ya wazao
wa Loti.’’
20 (Hiyo pia ilidhaniwa kuwa nchi ya Warefai
waliokuwa wakiishi huko, lakini Waamoni
waliwaita Wazamzumi. 21 Walikuwa watu wenye
nguvu na wengi, warefu kama Waanaki,
BWANA akawaangamiza kutoka mbele ya
Waamoni, ambao waliwafukuza na kukaa
mahali pao. 22 BWANA alikuwa amefanya hivyo
kwa wazao wa Esau, ambao waliishi Seiri,
wakati alipowaangamiza Wahori watoke mbele
yao. Waliwafukuza na wao wakaishi mahali pao
mpaka leo. 23 Nao Waavi ambao waliishi katika
vijiji mpaka Gaza, Wakaftori waliokuja kutoka
Kaptori waliwaangamiza na kukaa mahali pao.)
Kushindwa Kwa Sihoni Mfalme Wa
Heshboni
24 ‘‘Ondoka sasa na uvuke bonde la Arnoni.
Tazama, nimemweka Sihoni Mwamori mikononi
mwako, mfalme wa Heshboni na nchi yake.
Anza kuimiliki nchi hiyo na umwingize katika
vita. 25 Siku hii ya leo nitaanza kuwatia hofu na
woga mataifa yote chini ya mbingu wawaogope
ninyi. Watakaposikia taarifa zenu, watatetemeka
na kufadhaika kwa sababu yenu.’’
26 Kutoka jangwa la Kedemothi nilituma
wajumbe wenye maneno ya amani kwa Sihoni
mfalme wa Heshboni kusema, 27 ‘‘Turuhusu
tupite katika nchi yako. Tutapita katika barabara
kuu, hatutageuka kuume wala kushoto. 28 Tuuzie
chakula tule na maji tunywe kwa thamani yake
katika fedha. Turuhusu tu tupite kwa miguu,
29 kama wazao wa Esau ambao wanaishi Seiri
na Wamoabu ambao wanaishi Ari
walivyotufanyia, mpaka tuvuke Yordani kuingia
nchi ambayo BWANA Mungu wetu anatupatia.’’
30 Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni alikataa
kuturuhusu kupita. Kwa kuwa BWANA Mungu
wako ameifanya roho yake kuwa ngumu na
moyo wake kuwa mkaidi ili amweke kwenye
mikono yenu, kama alivyofanya sasa.
31 BWANA akaniambia, ‘‘Tazama, nimeanza
kuwapa mfalme Sihoni na nchi yake. Sasa
anzeni kuishinda na kuimiliki nchi yake.’’
32 Wakati Sihoni pamoja na jeshi lake lote
walipokuja kukutana nasi katika vita huko
Yahazi, 33 BWANA Mungu wetu alimweka
mikononi mwetu nasi tukamwangamiza pamoja
na wanawe na jeshi lake lote. 34 Kwa wakati ule
tuliteka miji yake yote na kuiangamiza kabisa:
wanaume, wanawake na watoto. Hatukubakiza
mtu hata mmoja. 35 Lakini mifugo na nyara
tulizoziteka kutoka ile miji tulijichukulia
wenyewe. 36 Kutoka Aroeri kwenye ukingo wa
bonde la Arnoni, kutoka mji ulio ndani ya bonde,
hata mpaka Gileadi hapakuwa na mji hata
mmoja uliokuwa na nguvu kutushinda. BWANA
Mungu wetu alitupa yote. 37 Lakini kulingana na
amri ya BWANA Mungu wetu, hamkujiingiza
katika nchi yo yote ya Waamori, wala katika
sehemu yo yote iliyo kando kando ya mto
Yaboki au katika miji iliyoko katika vilima, au
po pote pengine alipotukataza BWANA Mungu
wetu.
Kushindwa Kwa Ogu Mfalme Wa Bashani
Kisha tukageuka tukakwea kufuata
barabara iliyoelekea Bashani, Ogu mfalme
wa Bashani akaondoka na jeshi lake lote
kupigana na sisi huko Edrei. 2 BWANA
akaniambia, “Usimwogope kwa kuwa
nimekwisha mkabidhi mikononi mwako pamoja
na jeshi lake lote na nchi yake. Umfanyie
sawasawa na ulivyomfanyia Sihoni mfalme wa
Waamori ambaye alitawala huko Heshboni.’’
3 Hivyo BWANA Mungu wetu pia akamweka
Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake
lote mikononi mwetu. Tuliwaangamiza wote,
hakubakia hata mmoja. 4 Wakati huo tuliteka miji
yake yote. Hakuna mji hata mmoja kati ya ile
sitini ambao hatukuuteka, yaani eneo lote la
Argobu, utawala wa mfalme Ogu katika Bashani.
5 Miji yote hii ilijengewa ngome zenye kuta ndefu
zenye malango na makomeo, pia kulikuwako na
vijiji vingi ambavyo havikujengewa kuta.
6 Tuliwaangamiza kabisa, kama tulivyomfanyia
Sihoni mfalme wa Heshboni, tukiangamiza kila
mji, wanaume, wanawake na watoto. 7 Lakini
wanyama wote wa kufuga pamoja na nyara
kutoka kwenye miji yao tulichukua vikawa vyetu.
8 Hivyo kwa wakati huo tukachukua kutoka
kwa wafalme hawa wawili wa Waamori nchi ya
mashariki ya Jordani, kutoka bonde la Arnoni
mpaka kufika kwenye Mlima Hermoni.
9 (Wasidoni huuita mlima huo Sirioni, na
Waamori huuita Seniri.) 10 Tuliteka miji yote
kwenye uwanda wa juu, Gileadi yote, Bashani
yote mpaka kufika Saleka na Edrei, miji ya
utawala wa mfalme Ogu huko Bashani.
11 Mfalme Ogu ndiye peke yake aliyesalia
miongoni mwa mabaki ya Warefai, kitanda
chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa
3
4
952103022.001.png
 
KUMBUKUMBU LA TORATI
dhiraa tis a a na upana wa dhiraa nn e b . Mpaka
sasa kinaweza kuonekana katika mji wa
Waamori wa Raba.)
Mgawanyo wa nchi mashariki ya Yordani .
12 Katika nchi tuliyoiteka wakati ule, niliwapa
kabila la Reubeni na Gadi eneo lililoko kaskazini
la Aroeri kando ya bonde la Arnoni na nusu ya
eneo la milima ya Gileadi pamoja na miji yake.
13 Kisha nusu ya kabila la Manase niliwapa
sehemu ya Gileadi iliyobaki pamoja na Bashani
yote ambayo ni utawala wa Ogu. (Eneo lote la
Argobu katika Bashani lilikuwa linajulikana kama
nchi ya Warefai, 14 Yairi mzao wa kabila la
Manase, alichukuwa eneo lote la nchi ya Argobu
hadi kufikia mpaka wa Wageshuri na Wamaaka,
ukaitwa kwa jina lake, kwa hiyo mpaka leo hii
Bashani inaitwa Hawath-yairi.) 15 Nikampa Makiri
nchi ya Gileadi. 16 Lakini niliwapa Wareubeni na
Wagadi eneo kuanzia Gileadi hadi bonde la
Arnoni, (katikati ya bonde ulikuwa ndio mpaka,)
kuelekea mpaka mto Yaboki, ambao ndio
mpaka wa Waamoni. 17 Kwa upande wa
magharibi mpaka wao ulikuwa Yordani katika
Araba, toka ziwa Galilaya hadi bahari ya Araba,
(yaani Bahari ya chumvi), kwenye mitelemko ya
Pisga.
18 Wakati huo nilikuamuru: “BWANA Mungu
wako amekupa nchi hii uimiliki. Lakini ni lazima
wanaume wenu wote wenye uwezo, wakiwa
wamejiandaa tayari kwa vita, wavuke ng’ambo
ya pili wakiwatangulia ndugu zako Waisraeli.
19 Lakini wake zenu, watoto wenu na mifugo
yenu, (kwani najua mnayo mifugo mingi,)
wanaweza kukaa katika miji niliyowapa, 20 mpaka
hapo BWANA atakapowapa ndugu zenu
kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia
wamiliki ile nchi ambayo BWANA Mungu wenu
anawapa, ng’ambo ya Yordani. Baada ya hapo,
kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki
niliyowapa.”
23 Wakati huo nilimsihi BWANA: 24 “Ee
BWANA Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi
wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza.
Kwa kuwa ni mungu yupi aliyeko mbinguni au
duniani anayeweza kufanya kazi na matendo
makuu kama ufanyayo wewe? 25 Acha niende
nikaione hiyo nchi nzuri ng’ambo ya Yordani, ile
nchi nzuri ya vilima na Lebanoni.’’
26 Lakini kwa sababu yenu BWANA
alinikasirikia na hakutaka kunisikiliza. BWANA
aliniambia, “Hilo latosha usiseme nami jambo hili
tena. 27 Kwea juu ya kilele cha Pisga uangalie
magharibi, kaskazini, kusini na mashariki.
Iangalie hiyo nchi kwa macho yako, kwa vile
wewe hutavuka Yordani. 28 Lakini mwagize
Yoshua, mtie moyo na umtie nguvu, kwa kuwa
yeye atawaongoza watu hawa hadi ng’ambo na
kuwarithisha nchi utakayoiona.’’ 29 Kwa hiyo
tulikaa kwenye bonde karibu na Beth-peori.
Waa
mriwa Utii
4
Sikia sasa, Ee Israeli, amri na sheria
nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate
kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayo BWANA
Mungu wa baba zako anawapa. 2 Usiongeze
wala usipunguze cho chote ninachowaamuru
ninyi, ila myashike maagizo ya BWANA Mungu
wenu ambayo nawapa.
3 Mliona kwa macho yenu wenyewe kile
BWANA alichokifanya kule Baali-Peori. BWANA
Mungu wenu aliwaharibu kutoka miongoni
mwenu kila mmoja aliyemfuata Baali wa Peori,
4 lakini ninyi nyote mlioshikamana na BWANA
kwa uthabiti, Mungu wenu, mko hai mpaka leo.
5 Tazama, nimewafundisha amri na sheria
kama BWANA Mungu wangu alivyoniamuru
mimi, ili mzifuate katika nchi mnayoingia
kuimiliki. 6 Zishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii
itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa
mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi,
nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu
wenye hekima na ufahamu.’’ 7 Ni taifa gani
jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu
yao iliyo karibu nao kama BWANA Mungu wetu
alivyo karibu nasi wakati wo wote
tunapomwomba? 8 Nalo ni taifa gani jingine lililo
kubwa hivi lenye kuwa na amri na sheria za haki
kama hizi ninazoweka mbele yenu leo?
9 Mwe waangalifu, na makini ili msije
mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa
macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni
mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe
hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.
Mose Akataliwa kuvuka Yordani
21 Wakati huo nilimwamuru Yoshua,
“Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale
yote ambayo BWANA Mungu wenu
amewafanyia wafalme hawa wawili. BWANA
atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo
hivyo. 22 Msiwaogope, BWANA Mungu wenu
atapigana kwa ajili yenu.”
a 11 Dhiraa tisa ni sawa na mita 4.
b 11 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.
5
952103022.002.png 952103022.003.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin