1JN_Kiswahili_1068.pdf

(46 KB) Pobierz
1Yohana
Utangulizi
Yale yaliyomo katika waraka huu, mfano uandishi wake na ile misamiati iliyotumika vinakubaliana na lile
hitimisho kwamba nyaraka hizi ziliandikiwa wasomaji wale wale wa Injili ya Yohana. Waraka huu wa Kwanza
unakuwa kama ufupisho unaowawazia wasomaji kwamba tayari wanaijua Injili ya Yohana na unawahakikishia juu
ya imani yao katika Kristo. Waraka huu unaonyesha kuwa wasomaji walikuwa wanakabiliwa na upotovu wa imani
ya Unostiki, ambao ulikuja kuwa tatizo kubwa zaidi katika karne ya pili. Unostiki ulikuwa na mafundisho
yasemayo kwamba vitu vyote ni viovu lakini roho tu ndiyo nzuri.
Wazo Kuu
Katika ujumbe wa Injili, Yohana anaonyesha wazi kuwa Yesu ni Mungu aliyefanyika mwili na hivyo kupinga
kabisa ile dhana kwamba Kristo aliwaziwa tu kama aliyekuwa na mwili, eti kwamba Yeye alikuwa roho. Pia
iliondolea mbali yale mafundisho yaliyomwelezea Yesu kama vitu viwili, kwamba wakati fulani alikuwa anafanyika
mwanadamu na wakati mwingine anakuwa Mungu.
Mwandishi
Waraka wa Kwanza, wa Pili na wa Tatu wa Yohana tangu mwanzo kabisa zimeonekana kuwa mwandishi ni
mtume Yohana ambaye pia ndiye mwandishi wa Injili ya Yohana ,yaani, mojawapo ya zile Injili nne. Huyu ndiye
yule mwanafunzi aliyekuwa anapendwa ambaye aliegama kifuani mwa Yesu wakati wa chakula cha mwisho na
wanafunzi Wake.
Tarehe
Vitabu vyote hivi vinne, yawezekana vimeandikwa wakati mmoja, huenda kati ya 85-96 BK.
Mgawanyo
Utangulizi (1:1-4)
Umuhimu wa nuru katika ushirika (1:5-2:29)
Upendo sharti uenee katika maisha (3:1-4:21)
Imani na kuona kwa hakika (5:1-21)
1
1Yohana
Amri Mpya
7 Wapenzi, siwaandikii ninyi amri mpya bali
ile ya zamani, ambayo mmekuwa nayo tangu
mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno
mlilosikia. 8 Lakini ninawaandikia amri mpya,
yaani, lile neno lililo kweli ndani yake na ndani
yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya
kweli tayari inang’aa.
9 Ye yote anayesema yumo nuruni lakini
anamchukia ndugu yake bado yuko gizani.
10 Yeye ampendaye ndugu yake anakaa nuruni,
wala hakuna kitu cho chote ndani yake cha
kumkwaza. 11 Lakini ye yote amchukiaye ndugu
yake yuko gizani na anaenenda gizani, wala
hajui
Neno La Uzima
Tunawajulisha lile lilokuwako tangu
mwanzo, lile tulilosikia,ambalo tumeliona
kwa macho yetu, ambalo tumelitazama na
kuligusa kwa mikono yetu, kuhusu Neno la
Uzima, 2 Uzima huo ulidhihirishwa, nasi
tumeuona na kuushuhudia, nasi
twawatangazieni uzima wa milele, ambao
ulikuwa pamoja na Baba, nao ukadhihirishwa
kwetu. 3 Twawatangazia lile tuliloliona na
kulisikia ili kwamba nanyi mwe na ushirika nasi
na ushirika wetu hasa ni pamoja na Baba na
Mwanawe Yesu Kristo. 4 Tunaandika mambo
haya ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
1
anakokwenda,
kwa
sababu
giza
Kutembea Nuruni
5 Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka Kwake
na kuwatangazia ninyi, kwamba Mungi ni nuru
na ndani yake hamna giza lo lote. 6 Kama
tukisema kwamba twashirikiana naye huku
tukienda gizani, wasema uongo,wala hatutendi
lililo kweli. 7 Lakini tikienenda nuruni, kama Yeye
alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na
damu yake Yesu, Mwana Wake yatusafisha
dhambi yote.
8 Kama tukisema kwamba hatuna dhambi,
twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani
yetu. 9 Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi
zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu wote.
10 Kama tukisema hatukutenda dhambi,
twamfanya Yeye kuwa mwongo na Neno Lake
halimo ndani yetu.
limempofusha macho.
12 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo,
kwa sababu dhambi zenu zimesamehewa
kwa ajili ya Jina Lake.
13 Nawaandikika ninyi, akina baba,
kwa sababu mmemjua Yeye aliye tangu
mwanzo.
Nawaandikia ninyi vijana
kwa sababu mmemshinda yule mwovu.
Nawaandikia ninyi watoto wadogo,
kwa sababu mmejua Baba.
14 Nawaandikia ninyi akina baba,
kwa sababu mmejua Yeye aliye tangu
mwanzo.
Nawaandikia ninyi, vijana,
kwa sababu mna nguvu na neno la
Mungu linakaa ndani yenu,
nanyi mmeshinda yule mwovu.
Kristo Mwombezi Wetu
Watoto wangu wapendwa, nawaandikieni
haya ili msitende dhambi. Lakini kama
mtu ye yote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi
kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye haki. 2 Yeye
ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi
zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia
kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.
3 Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua
kama tunazishika amri Zake. 4 Mtu ye yote
asemaye kuwa, “Ninamjua” lakini hazishiki amri
Zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo
hamna kweli. 5 Lakini kama mtu ye yote analitii
Neno Lake, upendo wa Mungu umekamilika
ndani yake kweli kweli .Katika hili twajua kuwa
tumo ndani yake. 6 Ye yote anayesema anakaa
ndani Yake hana budi kuenenda kama Yesu
alivyoenenda.
Msiupende Ulimwengu
15 Msiupende ulimwengu wala mambo
yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu ye yote
akiupenda ulimwengu, kumpenda Baba hakumo
ndani yake. 16 Kwa maana kila kitu kilichomo
ulimwenguni, yaani, tamaa ya mwili, tamaa ya
macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba
bali hutokana na ulimwengu. 17 Nao ulimwengu
unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye
afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.
2
Onyo Dhidi Ya Mpinga Kristo .
18 Watoto wadogo, huu ni wakati wa
mwisho! Kama mlivyosikia kwamba mpinga
Kristo anakuja, hivyo basi wapinga Kristo wengi
wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua
kwamba huu ni wakati wa mwisho. 19 Walitoka
2
952117484.003.png
 
1Yohana
kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa
maana kama wangelikuwa wa kwetu,
wangelikaa pamoja nasi, lakini kutoka kwao
kulionyesha kwamba hakuna hata mmoja wao
aliyekuwa wa kwetu.
20 Lakini ninyi mmetiwa mafuta na Yeye
Aliye Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli.
21 Siwaandikii kwa sababu hamjui kweli, bali kwa
sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo
utokao katika kweli. 22 Je, mwongo ni nani?
Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si
Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo,
yaani, yeye humkana Baba na Mwana.
23 Hakuna ye yote amkanaye Mwana aliye na
Baba. Ye yote anayemkubali Mwana anaye na
Baba pia.
24 Hakikisheni kwamba lile mlilosikia tangu
mwanzo linakaa ndani yenu. Kama lile mlilosikia
tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi ninyi
mtakaa ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25 Hii
ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele.
26 Ninawaandikia mambo haya kuhusu wale
watu ambao wanajaribu kuwapotosha. 27 Kwa
habari yenu ninyi, upako ule mlioupata kutoka
Kwake unakaa ndani yenu, wala ninyi hamna
haja ya mtu ye yote kuwafundisha. Lakini kama
vile upako Wake unavyowafundisha kuhusu
mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi
kama ulivyowafundisha kaeni ndani Yake.
atendaye dhambi hakumwona Yeye wala
hakumtambua.
7 Watoto wadogo, mtu ye yote na
asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana
haki, kama Yeye alivyo na haki. 8 Yeye atendaye
dhambi ni wa Ibilisi, kwa sababu Ibilisi amekuwa
akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili
Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziangamize
kazi za Ibilisi. 9 Ye yote aliyezaliwa na Mungu
hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu
wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi
kwa sababu amezaliwa na Mungu. 10 Kwa jinsi
hii tunaweza kujua dhahiri watoto wa Mungu na
watoto wa Ibilisi nao. Ye yote asiyetenda haki
hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda
ndugu yake.
Mpendane Ninyi Kwa Ninyi .
11 Hili ndilo neno mlilolisikia tangu mwanzo,
kwamba imetupasa tupendane sisi kwa sisi.
12 Msiwe kama Kaini aliyekuwa wa yule mwovu
akamwua ndugu yake. Basi kwa nini alimwua?
Ni kwa sababu matendo yake Kaini yalikuwa
mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
13 Ndugu zangu, ninyi msistaajabu kama
ulimwengu ukiwachukia. 14 Sisi tunajua ya
kwamba tumepita kutoka mautini kuingia
uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila
asiyempenda ndugu yake akaa mautini. 15 Ye
yote amchukiaye ndugu yake ni mwuaji, nanyi
mwajua ya kwamba mwuaji hana uzima wa
milele ndani yake.
16 Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la
Mungu, kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai
Wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai
kwa ajili ya hao ndugu. 17 Ikiwa mtu anavyo vitu
vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake
ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu
wakaaje ndani ya mtu huyo? 18 Watoto wangu
wadogo, tusipende kwa maneno au kwa ulimi
bali kwa tendo na katika kweli. 19 Basi hivi ndivyo
tutakavyoweza kujua ya kuwa sisi tu wa kweli
na hivyo twaithibitisha mioyo yetu mbele za
Mungu 20 kila mara mioyo yetu inapotuhukumu.
Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu,
naye anajua kila kitu.
21 Wapenzi, kama mioyo yetu haituhukumu,
tunao ujasiri mbele za Mungu. 22 Lo lote
tuombalo, twalipokea kutoka Kwake, kwa
sababu tumezitii amri Zake na kutenda yale
yanayompendeza. 23 Hii ndiyo amri Yake,
kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Yesu Kristo
na kupendana sisi kwa sisi kama Yeye
Watoto Wa Mungu
28 Sasa basi, watoto wadogo, kaeni ndani
Yake, ili atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala
tusiaibike mbele zake wakati wa kuja kwake.
29 Kama mkijua kuwa Yeye ni mwenye haki,
mwajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa
na Yeye.
Oneni ni pendo kuu namna gani alilotupa
Baba, kwamba sisi tuitwe watoto wa
Mungu! Nasi ndivyo tulivyo. Sababu kwa nini
ulimwengu haututambui, ni kwa kuwa
haukumtambua Yeye. 2 Wapenzi, sasa tu watoto
wa Mungu, lakini bado haijadhihirika
tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba, Yeye
atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa
maana tutamwona kama alivyo. 3 Kila mmoja
mwenye matumaini haya katika Yeye
hujitakasa, kama vile Yeye alivyo mtakatifu.
4 Kila mtu atendaye dhambi afanya uasi,
kwa kuwa dhambi ni uasi. 5 Lakini mwajua ya
kuwa Yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi,
wala ndani Yake hamna dhambi. 6 Kila mtu
akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila mtu
3
3
952117484.004.png
 
1Yohana
alivyotuamuru. 24 Wale wote wanaozishika amri
Zake hukaa ndani Yake na Yeye ndani yao. Hivi
ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu.
Nasi twajua hili kwa njia ya Roho yule
aliyetupatia.
upendo wa Mungu alio nao kwa ajili yetu.
Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo
hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani
yake. 17 Kwa njia hii, upendo hukamilishwa
miongoni mwetu ili tupate kuwa na ujasiri katika
siku ya hukumu, kwa sababu kama alivyo
ndivyo tulivyo sisi katika ulimwengu huu.
18 Katika upendo hakuna hofu. Lakini upendo
ulio kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu
inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu
hakukamilika katika upendo. 19 Twampenda
Yeye kwa sababu Yeye alitupenda kwanza.
20 Ikiwa mtu atasema,”Nampenda Mungu”, lakini
anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa
maana kila mtu asiyempenda ndugu yake
ambaye amemwona, atampendaje Mungu
ambaye hajamwona? Naye ametupa amri hii:
Ye yote anayempenda Mungu lazima pia
ampende ndugu yake.
Zijaribuni Hizo Roho
Wapenzi, msiamini kila roho,bali zijaribuni
hizo roho mwone kama zimetoka kwa
Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo
wametokea ulimwenguni. 2 Hivi ndivyo
mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila
roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja
katika mwili yatoka kwa Mungu. 3 Lakini kila roho
ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii
ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia
kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.
4 Watoto wadogo, ninyi mmetokana na
Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu Yeye
aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika
ulimwengu. 5 Wao wanatokana na ulimwengu na
kwa hiyo hunena yaliyo ya ulimwengu, hivyo
ulimwengu huwasikia. 6 Sisi twatokana na Mungu
na ye yote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini
asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo
tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho
ya upotovu.
4
Imani Katika Mwana Wa Mungu Huushinda
Ulimwengu
Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye
Kristo amezaliwa na Mungu na ye yote
ampendaye Baba humpenda pia mtoto
aliyezaliwa naye. 2 Hivi ndivyo tunavyojua
kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, kwa
kumpenda Mungu na kuzitii amri Zake. 3 Kwa
kuwa huu ndio upendo wa Mungu, kwamba
tuzitii amri Zake. Nazo amri Zake si nzito. 4 Kwa
maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda
ulimwengu. Huku ndiko kuushinda kuushindako
ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu. 5 Ni nani yule
aushindaye ulimwengu? Ni yule aaminiye
kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
5
Mungu Ni Upendo
Wapenzi na tupendane, kwa kuwa upendo
watoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa
na Mungu naye anamjua Mungu. 8 Yeye
asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu
ni upendo. 9 Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha
upendo Wake kwetu, kwa sababu Mungu
alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili
tupate uzima kwa Yeye. 10 Huu ndio upendo, si
kwamba tulimpenda Mungu, bali Yeye
alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili Yeye awe
dhabihu ya kipatanisho kwa ajili ya dhambi zetu.
11 Wapenzi, kama Mungu alitupenda sisi hivi,
imetupasa na sisi kupendana. 12 Hakuna mtu ye
yote aliyemwona Mungu wakati wo wote. Kama
tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu na
upendo Wake umekamilika ndani yetu.
13 Tunajua kwamba twakaa ndani Yake na
Yeye ndani yetu, kwa sababu ametupatia sisi
sehemu ya Roho Wake. 14 Nasi tumeona na
kushuhudia kwamba Baba amemtuma
Mwanawe ili awe Mwokozi wa ulimwengu. 15 Kila
akiriye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu,
Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya
Mungu.
Ushuhuda Kuhusu Mwana Wa Mungu
Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu,
yaani, Yesu Kristo. Hakuja kwa maji peke yake,
bali kwa maji na damu. Naye Roho ndiye
ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.
7 Kwa maana wako watatu washuhudiao
mbinguni:Hao ni Baba, Neno na Roho Mtakatifu,
nao hawa watatu ni wamoja. 8 Pia wako
mashahidi watatu duniani, yaani, Roho, Maji na
Damu, wote hawa watatu wanakubaliana katilka
umoja. 9 Kama tunaukubali ushuhuda wa
wanadamu, basi ushuhuda wa Mungu ni mkuu
zaidi, kwa kuwa huu ndio ushuhuda wa Mungu
kwamba amemshuhudia Mwanawe. 10 Kila mtu
amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda
ndani mwake.Kila mtu asiyemwamini Mungu
amemfanya Yeye kuwa mwongo, kwa sababu
16 Hivyo nasi twajua na kuutumainia
4
952117484.001.png
 
1Yohana
hakuamini ushuhuda Mungu alioutoa kuhusu
Mwanawe. 11 Huu ndio ushuhuda kwamba,
Mungu ametupa uzima wa milele, nao huo
uzima umo katika Mwanawe. 12 Aliye naye
Mwana wa Mungu anao uzima,yeye asiye na
Mwana wa Mungu hana uzima.
Maneno Ya Mwisho
13 Nawaandikia mambo haya ninyi
mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu ili mpate
kujua ya kuwa mnao uzima wa milele. 14 Huu
ndio ujasiri tulio nao ndani Yake, kama tukiomba
kitu sawasawa na mapenzi Yake, atusikia.
15 Nasi kama tunajua ya kuwa atusikia, lo lote
tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha
kupata zile haja tulizomwomba.
16 Kama mtu akimwona ndugu yake
anatenda dhambi isiyo ya mauti, inampasa
aombe, naye Mungu atampa uzima mtu
huyo,yaani, kwa wale ambao dhambi yao si ya
mauti. Iko dhambi ya mauti, sisemi kwamba
utaomba kwa ajili ya hiyo. 17 Jambo lo lote lisilo
la haki ni dhambi, lakini iko dhambi isiyo ya
mauti.
18 Tunajua ya kuwa yeye aliyezaliwa na
Mungu hatendi dhambi, bali aliyezaliwa na
Mungu hujilinda wala yule mwovu hawezi
kumdhuru. 19 Sisi twajua kuwa tu watoto wa
Mungu na ya kwamba ulimwengu wote uko chini
ya utawala wa yule mwovu. 20 Nasi twajua ya
kwamba Mwana wa Mungu amekuja, naye
ametupa sisi akili ili tupate kumjua Yeye aliye
Kweli. Nasi tumo ndani Yake Yeye aliye Kweli,
yaani, ndani ya Yesu Kristo Mwanawe. Yeye
ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele.
21 Watoto wadogo,jilindeni na sanamu.
Amen.
5
952117484.002.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin